Alicho Kiandika Msanii @officialshilole
''Naandika
haya, nikiwa na akili timamu na utulivu, La kwanza kabisa nataka KUOMBA
RADHI JAMII YANGU. Naomba radhi kwa sababu niliwaaminisha ndoa yangu
haina tatizo, huku ukweli ukiwa hauko hivyo, nimekuwa mtu wa kuambulia
vipigo na MENGINE yasiyozungumzika, Naomba radhi kwa sababu niliposikia
wanawake wenzangu wakipigwa niliwaambia PAZENI SAUTI, niliposikia
mwanamke kule Kigamboni ameuwawa na kuchomwa moto niliomboleza na jamii
na kusema Bora angesema".. huku mimi nikijikausha na kujitoa kwenye
kundi lao wakati ukweli wangu MIMI NI MWENZAO, Naomba radhi.
Mimi ni kioo cha jamii, tena sura kubwa ya wanawake.
Leo numeona nivunje ukimya kwa kuweka wazi kwamba MUME WANGU ASHRAFU
SADIKI, maarufu kama UCHEBE AMEKUWA ANANIPIGA SAAANA, na tena hata baada
ya kunipiga hajali kupiga simu wala kujua naendeleaje, nauguzwa na watu
baki hospitali, na bado manyanyaso mengine yanayoikosesha hii
ninayoiita Ndoa uhai na furaha
na zaidi nina WATOTO, watoto wanaoniangalia kama Baba na Mama, leo nikubali kufa na kuacha wanangu barabarani, SITAWEZA
.
'Uchebe'
ni mwanaume niliyempenda, nilimvumilia kwa madhaifu yote, nikampa kila
kitu, (Utu wangu, Mali Zangu na hata palipotakiwa kumuendeleza asimame
mwenyewe nilifanya kwakuwa nilijua tuko pamoja), lakini HILO HALIKUWAHI
KUZUIA VIPIGO, DHARAU NA USALITI.
.
Siku 2
zilizopita baada ya kutoka SABASABA KUTAFUTIA WATOTO WANGU NA KUMTAFUTIA
YEYE NILIPIGWA SANA. SABABU ZA KUPIGWA NI MIGOGORO MIDOGO YA KAWAIDA
AMBAYO IPO KWENYE KILA NDOA, sio kwamba amenifumania au mambo
yanayoshindwa kuzungumzika, hapana, Tena Namuheshimu sana, lakini
solution aliyoiona ni kunipiga kinyama bila huruma, tena kwa kunishtua
na ngumi nikiwa usingizini, Kama mnavyoona picha hapo ni matukio ya siku
tofauti tofauti.
Najua nitalaumiwa kwa kuweka
hili mtandaoni, ILA SINA NAMNA, MAISHA YANGU NI MAISHA YA WATU KWA KIASI
KIKUBWA, JAMII INANITAZAMA KAMA MFANO.. Nimefika mwisho, na kuanzia
sasa naomba nisitambulike kama Mke wa Uchebe, ila Mama alieamua kuweka
maslahi ya watoto wake mbele na kuamua kuwa mwenyewe kwa usalama na
furaha yake, Wakati nahangaikia mambo yangu ya ndoa, post hii itumike
kuwakumbusha wanawake"


Comments
Post a Comment